IQNA

Kiongozi Muadhamu: Maendeleo ya nchi yanategemea "nguzo pacha za elimu na kuchapa kazi"

13:43 - May 02, 2026
Habari ID: 3482189
IQNA-Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameapa kuwa taifa la Iran litamshinda pia adui katika nyanja za kiutamaduni na kiuchumi baada ya kupata ushindi katika medani ya vita vya kijeshi.

Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei ameyasema hayo katika ujumbe wake siku ya Ijumaa kwa mnasaba wa maahimisho ya Siku ya Mwalimu na Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi.

"Hivi Sasa, ambapo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, baada ya zaidi ya miaka 47 ya mapambano, imeuthibitishia ulimwengu sehemu ya uwezo wake wa ajabu katika vita vya kijeshi dhidi ya maadui wa maendeleo na ustawi kwa kutegemea neema ya Mwenyezi Mungu, inapasa pia kuwakatisha tamaa na kuwashinda katika awamu ya Jihadi ya kiuchumi na kiutamaduni," ameandika Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei pia amesema: "Walimu watakuwa kiungo chenye ushawishi mkubwa katika vita vya kitamaduni, na wafanyakazi watakuwa sehemu ya ufanisi zaidi katika vita vya kiuchumi-kiasi kwamba tunaweza kusema kuwa wawili hawa wanatumika kama uti wa mgongo katika nyanja za utamaduni na uchumi,"

Tarehe 2 Mei, Iran imeadhimisha Siku ya Taifa ya Walimu, ambayo inasadifiana na kumbukumbu ya kuuawa shahidi mwanazuoni mashuhuri wa Iran, Ayatullah Morteza Mutahhari. Wakati huo huo, Siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi Duniani, inaadhimishwa kila mwaka kila ifikapo tarehe Mosi mwezi Mei.

Kiongozi Muadhamu amesema kuwa maendeleo ya nchi yanategemea "nguzo pacha za elimu na kuchapa kazi," na ametoa wito wa kuungwa mkono kivitendo kwa makundi yote mawili.

Akitotoa ufafanuzi, Ayatullah Mojtaba Khamenei amesema: Waalimu, wanabeba "jukumu zito" la ustadi wa kufundisha, kukuza uelewa, na kuunda utambulisho wa kizazi kijacho.

Ayatullah Khamenei amewaonya maafisa wa serikali kwamba kutoa heshima za maneno tu hakutoshi na kusisitiza kuwa: "Kama ambavyo taifa la Iran limeonyesha uungaji mkono unaostahili kwa vikosi vyao vya jeshi, inafaa pia waonyeshe uungaji mkono mkubwa kwa walimu na wafanyakazi."

Ametoa wito wa mwingiliano mkubwa kati ya familia na wasimamizi wa shule, na amewasihi raia kuweka kipaumbele kwenye bidhaa zinazotengenezwa ndani ya nchi ili kuwasaidia wafanyakazi wa ndani.

3497301

captcha