IQNA

Uchunguzi wa mifumo ya uandishi katika elimu ya kiraa mbalimbali za Qur'ani nchini Oman

10:40 - December 03, 2008
Habari ID: 1715375
Kongamano la kimataifa lililochunguza Mifumo ya Uandishi wa Elimu ya Kiraa za Qur'ani limefanyika katika Kitivo cha Fasihi na Elimu Jamii cha Chuo Kikuu cha Sultan Qabus mjini Mascut, Oman.
Kongamano hilo lilijadili maudhui za utambuzi zaidi wa wasomi wa Qur'ani kuhusu aina mbalimbali za kiraa za Qur'ani, maarifa ya elimu ya kiraa na tajwidi na umuhimu wake kwa wanafunzi wa lugha na fasihi ya Kiarabu na sayansi ya Qur'ani na uchunguzi wa mirengo ya uandishi katika elimu ya kiraa mbalimbali za Qur'ani.
Mhadhiri wa lugha ya Kiarabu katika Kitivo cha Fasihi cha Chuo Kikuu cha Sultan Qabus Mustafa Adnan ambaye alihutubia kongamano hilo amesema kuwa fani za kiraa mbalimbali za Qur'ani, tajwidi na maisha ya wasomaji Qur'ani ni sehemu ya mifumo ya elimu ya kiraa ya Qur'ani na kwamba watafiti wanaweza kuandika vitabu vya thamani katika medani hiyo. Mustafa Adnan amesema kuwa elimu ya kiraa za Qur'ani ni marejeo muhimu kwa wanafunzi wa fani ya lugha na fasihi ya Kiarabu na wanafunzi wa sayansi ya Qur'ani na akaongeza kuwa elimu hiyo ni marejeo ya kutegemewa katika somo la sarufi na utambuzi wa lugha.
Amesema kuwa katika kipindi cha sasa kuna vitabu vichache vinavyozungumzia elimu za kiraa mbalimbali za Qur'ani muhimu zaidi kikiwa ni kitabu cha al Hujja fil Qiraatis Sab'i kilichoandikwa na Hassan bin Ahmad bin Khalwaihi aliyezaliwa mwaka 370 Hijria. 329004

captcha