IQNA

Zaidi ya visa 29,000 za Hija zatolewa kwa Mahujaji wa Iran kwa ushirikiano wa Saudia

13:33 - May 06, 2026
Habari ID: 3482208
IQNA – Wakati mchakato wa kuwasafirisha waumini wa Iran kuelekea Saudi Arabia kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Hija ukiendelea kushika kasi, idadi kubwa ya visa za Hija kwa waumini hao tayari zimetolewa.

Kwa mujibu wa Kituo cha Habari cha Hija na Ziara; kutokana na ufuatiliaji wa karibu unaofanywa na Ofisi ya Mwakilishi wa Shirika la Hija na Ziara la Iran nchini Saudi Arabia, hadi sasa visa 29,326 za Hija zimetolewa kwa waumini wa Iran wanaoelekea katika ibada ya Hija mwaka huu.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mchakato wa kupata visa zilizosalia unaendelea kwa bidii, huku misafara ikiendelea kuondoka kwa utaratibu. Aidha, ushirikiano na msaada wa maafisa wa Wizara ya Hija na Umra ya Saudi Arabia, akiwemo Naibu Waziri wa Hija na Umra Abdul Fattah Mushat na Naibu Waziri wa Masuala ya Kimataifa Al-Hassan Manakhara, umechangia kwa kiasi kikubwa kuharakisha utoaji wa visa hizo.

Hadi sasa, takribani asilimia 40 ya waumini wa Iran waliojisajili kwa ajili ya ibada ya Hija mwaka huu tayari wamewasili katika Ardhi ya Wahyi, na zoezi la kuwasafirisha waliosalia linaendelea kwa mpangilio maalum.

Kwa mujibu wa maafisa, mwaka huu zaidi ya waumini 30,000 kutoka Iran watatekeleza ibada ya Hija.

Hija ni ibada kuelekea Makka Tukufu ambayo kila Muislamu mwenye uwezo wa kimwili na kifedha analazimika kuitekeleza angalau mara moja katika maisha yake.

Ibada hii ya kila mwaka inahesabiwa kuwa miongoni mwa nguzo za Uislamu na ni mkusanyiko mkubwa zaidi wa ibada ya pamoja duniani.

Vilevile, Hija ni dhihirisho la umoja wa Waislamu na unyenyekevu wao kwa Mwenyezi Mungu (Subhanahu wa Ta‘ala).

3497359

Kishikizo: hija saudi arabia iran
captcha