Mwandishi wa IQNA nchini Kyrgyzstan ameripoti kuwa wanafunzi wa madrasa ya Badr wanajifunza Qur’ani kwa kutumia kiraa mbalimbali kama ya Hafs, Warsh na Qalun, sayansi ya Qur’ani Tukufu na maarifa ya Kiislamu.
Elimu ya Qur’ani katika madrasa hiyo inatolewa na msomaji maarufu wa Kyrgyzstan Ustadh Qudratullah.
Mwanazuoni mkubwa wa Kyrgyzstan Sheikh Sadruddin vilevile anatoa masomo ya fiqhi na sarufi ya lugha ya Kiarabu katika madrasa hiyo. 332841