IQNA

Al Azhar yapasisha uchapishwaji wa tafsiri ya kwanza ya Qur'ani ya mwanamke

11:10 - December 20, 2008
Habari ID: 1720543
Taasisi ya Uhakiki wa Kiislamu ya Chuo Kikuu cha al Azhar nchini Misri imepaisha uchapishaji wa tafsiri ya kwanza ya Qur'ani iliyoandikwa na mwanamke.
Tafsiri hiyo iliyopewa jina la Taysirul Tafsir imeandikwa na Bibi Fauqiya Ibrahim al Sharbini wa Misri.
Tafsiri hiyo imeruhusiwa kuchapishwa baada ya kuchunguzwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu ya al Azhar.
Uchunguzi wa tafsiri hiyo ya Qur'ani yenye juzuu nne umechukua kipindi cha miaka mitatu.
Juzuu ya kwanza ya tafsiri hiyo inajunuisha sura za al Hamdu hadi Tauba, juzuu ya pili sura za Yunus hadi Haj, juzuu ya tatu inaanzia sura ya Muuminun hadi Zukhruf na juzuu ya nne inaanzia sura ya Dukhan hadi sura ya Nas.
Mwandishi wa tafsiri hiyo bi Fauqiya Ibrahim al Sharbini amesema: Uandishi wa tafsiri hiyo umechukua kipindi cha miaka saba na kwamba amesubiri kibali cha kuchapishwa kwake kwa miaka mitatu.
Bibi Fauqiya ambaye ana umri wa miaka 72 ameongeza kuwa, tafsiri hiyo imetegemea hadithi na vyanzo sahihi vya maulama na wasomi wa Kiislamu.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa wiki kadhaa zilizopita Wizara ya Sheria ya Misri ilimuidhinisha muadhini wa kwanza wa kike nchini humo, suala ambalo limezusha malalamiko na upinzani wa waadhini wa kiume. 335376
captcha