IQNA

Mkutano wa kimataifa wa Muujiza wa Kielimu wa Qur’ani na Suna kufanyika Saudi Arabia

12:14 - December 21, 2008
Habari ID: 1720998
Mkutano wa kimataifa wa Muujiza wa Qur’ani na Suna za Mtume Muhammad (saw) unatarajiwa kuanza tarehe 23 Disemba katika mji wa Dammam ulioko mashariki mwa Saudi Arabia.
Mkutano huo unasimamiwa na Kituo cha Sayansi na Teknolojia cha Sultan bin Abdulaziz kikishirikiana na Jumuiya ya Kimataifa ya Muujiza wa Kielimu wa Qur’ani na Suna za Mtume Mtukufu.
Mkutano huo utahudhuriwa na watafiti wa masuala ya Qur’ani kutoka nchi kadhaa za Kiislamu ikiwemo Yemen, Oman, Imarati na Saudi Arabia yenyewe.
Makala mbalimbali kuhusu historia na sheria za muujiza wa kielimu wa Qur’ani Tukufu zitawasilishwa katika mkutano huo. 335751



captcha