Taasisi ya Uchapishaji Quran ya Mfalme Fahd nchini Saudi Arabia imechapisha zaidi ya nuskha milioni 216 za Qur'ani, vitabu vingine na programu za kompyuta za Qur'ani kwa lugha 34 duniani tokea ilipozinduliwa mwaka 1984 hadi mwezi Novemba mwaka 2008 .
Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Habari za Kiislamu IINA, taasisi hiyo mwezi uliopita ilisambaza zaidi ya nuskha laki mbili za Qur'ani na vitabu vinavyohusu Qur'ani ambavyo vilionyeshwa katika maonyesho ya vitabu nchini Saudi Arabia na maeneo mengine duniani.
Taasisi ya Chapa na Uchapishaji Qur'an ya Mfalme Fahd mwezi wa Oktoba ilitambuliwa kama taasisi ya Kiislamu yenye harakati zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu na kutunukiwa zawadi ya kimataifa ya Qur'ani ya Dubai.
Ingawa Taasisi ya Uchapishaji Quran ya Mfalme Fahd huchukua nafasi ya kwanza kila mwaka katika uchapishaji na usambazaji Qur'ani na vitabu vingine vya kidini kama vile tafsiri, lakini baadhi shughuli za taasisi hiyo zinapaswa kuangaliwa kwa jicho la tahadhari kutokana na ushawishi wa Mawahabi katika vituo na taasisi mbalimbali nchini Saudi Arabia. 337229