IQNA

Tony Blair: Qur'ani imelitaja kwa heshima jina la Yesu Kristo

12:39 - December 25, 2008
Habari ID: 1722641
Kila siku ninasoma Qur'ani na ninauheshimu Uislamu na Waislamu. Wakristo wanadhani kwamba Waislamu wanawafanyia uhasa ilhali katika Qur'ani hakuna hata neno moja linalouvunjia heshima Ukristo na kitabu hicho kinalitaja kwa heshima kamili jina la Mtukufu Masiya.
Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair ambaye alikuwa muitifaki mkubwa wa Rais George Bush wa Marekani katika kuishambulia kijeshi Iraq hapo mwaka 2003. Blair ameyasema hayo katika mahojiano yake na gazeti moja la Ujerumani na kusisitiza kuwa, kuelewa na kufahamu itikadi za kidini za Waislamu kunaisadia jamii ya kimataifa katika kutatua matatizo na mivutano iliyopo hivi sasa!
Matamshi hayo yanatolewa na Tony Blair ambaye jumuiya za kisheria za Ulaya hivi karibuni zilitoa wito wa kufikishwa kwake mahakamani kwa tuhuma za kutenda jinai za kivita kutokana na kukiuka sheria za kimataifa na kushiriki katika mashambulizi haramu ya kijeshi dhidi ya Iraq.
Baada ya kung'atuka madarakani, Blair aliteuliwa kuwa mwakilishi wa kamati ya kimataifa ya pande nne ya mpango wa amani kwa ajili ya Mashariki ya Kati "Road Map", suala ambalo liliwashangaza walimwengu.
Kamati hiyo inaundwa na nchi za Marekani na Russia na Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa. 338028
captcha