Sayyid Ali Sarabi mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Muungano wa Jumuiya za Masuala ya Qur'ani amesema kuwa jumuiya hiyo itakuwa daraja la mawasiliano la kukusanya misaada ya wananchi wa Iran kwa ajili ya Wapalestina wanaouawa kinyama katika Ukanda wa Gaza.
Ali Sarabi amelaani mauaji ya umati yanayoendelea kufanywa na jeshi la utawala ghasibu wa Israel katika Ukanda wa Gaza na akasema: Waislamu wote wanawajibika kutekeleza majukumu yao mazito, kukabiliana na jinai za Wazayuni na kuwasaidia wananchi wa Palestina. Amesema kuwa ukatili wa Wazayuni dhidi ya wananchi wasiokuwa na hatia wa Palestina hauwezi kuhalalishwa kwa hali yoyote ile na ni ishara ya wahaka na kiwewe cha dola ghasibu la Israel na Marekani kuhusu nguvu zinazoongeka kila siku za Waislamu kote duniani.
Sayyid Ali Sarabi amesema: Hii leo Wapalestina wako mstari wa mbele wa mapambano ya Uislamu dhidi ya ukafiri na ni wajibu kwa wanadamu wote na Waislamu kuwatetea wananchi wanaodhulumika wa Ukanda wa Gaza. 340025