IQNA

Vipofu wa Bangladesh watunukiwa Qur'ani zenye hati ya Braille

13:55 - January 12, 2009
Habari ID: 1729663
Jumuiya ya Vipofu Bangladesh imetunukiwa nuskha kadhaa za Qur'ani Tukufu kwa hati za Braille.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Pakistan APP, Liyaqat Ali Khan Mkuu wa Baraza la Uwakilishi wa Pakistan katika mji mkuu wa Bangladesh, Dhaka, Jumamosi aliwakabidhi wakuu wa Jumuiya ya Vipofu Bangladesh nuskha hizo za Qur'ani zenye hati ya Braille.
Inatazamiwa kuwa maelfu ya vipofu nchini Bangladesh wataweza kunufaika na ujumbe wa Wahyi bila vizingiti.
Lengo la kuwatunuku vipovu wa Bangladesh Qur'ani zenye hati za Braille ni kuwawezesha kusoma kitabu hicho kitakatifu kwa kina na kufahamu maana yake.
Liyaqat Ali Khan amehutubu katika sherehe za kukabidhi misahafu hiyo na kusema: “Leo wengi wanataka kueneza taswira potofu kuhusu Uislamu na mafunzo ya dini hii tukufu ya mbinguni. Kwa kuzingatia hilo ni jambo la dharura kwa Waislamu wote kuufahamu Uislamu halisi ipasavyo”. 346210
captcha