Wairani vilevile walitunga vitabu vya kanuni za sarufi ya nahau ya lugha ya Kiarabu ili kuweza kufahamu vyema kitabu kitukufu cha Qur'ani.
Hayo yamesemwa na mhadhiri wa chuo kikuu Ghulamhussein Ibrahimi Dinani. Amesema katika kongamano la kimataifa la "Iran Utamaduni" lililofanyika kwenye Chuo Kikuu cha Tehran kwamba, wanazuoni wakubwa wa fiqhi na sheria za Kiislamu wa madhehebu za Shafi', Hanafi, Hanbali na Ja'fari walikuwa Wairani na vilevile waandishi wa vitabu vya hadithi kama sahihi sita zikiwemo Sahihi Bukhari na Muslim.
Mhadhiri huyo wa chuo kikuu ameongeza kuwa, Wairani waliandika vitabu vya nahau na sarufi ya lugha ya Kiarabu kwa ajili ya kuelewa vyema kitabu cha Qur'ani Tukufu. Ametoa mfano wa Sibawaihi ambaye ni miongoni mwa wanazuoni wakubwa na wataalamu wa fasihi ya Kiarabu. 347768