IQNA

Pakistan yapiga marufuku uchapishaji wa Qur'ani kwa kutumia karasi za daraja ya chini

12:16 - January 18, 2009
Habari ID: 1732462
Waziri wa Masuala ya Kidini wa Pakistan amepiga marufuku utumiaji wa karatasi za daraja ya chini kwa ajili ya kuchapisha nakala za Qur'ani Tukufu.
Kituo cha habari cha Thenews kimeripoti kuwa Hamid Said ameliambia bunge la nchi hiyo kwamba tokea sasa serikali itasimamia kwamakini viwango na ubora wa karatasi zinazotumiwa kuchapishia Qur'ani na kwamba wachapishaji wanaotumia karatasi zenye viwango vya chini watachukuliwa hatua za kisheria.
Waziri wa Masuala ya Kidini wa Pakistan amesema: Kwa sasa watu wanaochapisha Qur'ani kwa karatasi zisizokuwa na ubora unaohitajika wanapigwa faini ya rupia elfu tano na kifungo cha jela miaka mitatu na kwamba faini hiyo itaongezwa na kuwa rupia elfu 50. 349623
captcha