Katika makala yake iliyopewa anwani ya "Kushindwa Kimaadili", gazeti hilo limeandika kuwa: Kuharibu misikiti na vituo vya Qur'ani huko Gaza na kuchoma moto kitabu kitukufu cha Waislamu katika kipindi chote cha vita ni kitendo cha kinyama na kisichokuwa cha kimaadili kilichofanywa na askari wa Israel katika vita vya siku 22.
Gazeti hilo la Israel limeashiria kwamba nusu ya waliouawa katika mashambulizi ya Gaza walikuwa wanawake na watoto wadogo na kuhoji kwamba je, lengo la mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza lilikuwa ni kuangamiza harakati ya Hamas au kuvunjia heshima itikadi za Waislamu na kuwaua kwa umati watu wasiokuwa na hatia?
Mwishoni mwa makala hiyo, gazeti la Maariv la Israel limeandika: Kuna ushahidi madhibuti unaothibitisha kwamba jeshi la Israel lilikuwa likishambulia kwa makusudi makazi ya raia, shule na misikiti ya Gaza na kwamba taarifa ya jana ya jeshi la Israel lililokiri kwamba limetumia fosforasi nyeupe na mabomu ya joto katika vita vya Gaza imezitia wasiwai mkubwa jumuiya za kimataifa juu ya utumiaji wa silaha zilizopigwa marufuku. 352246