IQNA

Jamii ya Qur'ani nchini Iran kutangaza tena utiifu wake kwa hayati Imam Khomeini

8:16 - January 24, 2009
Habari ID: 1734730
Jamii ya Qur'ani nchini Iran Jumamosi ya leo itatangaza tena utiifu wake kwa thamani za muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayati Imam Khomeini sambana na kutimia mwaka wa 30 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Wawakilishi wa Jamii ya Qur'ani nchini Iran wanatazamiwa kutangaza tena utiifu wao kwa thamani za Imam Khomeini katika sherehe zinazoendelea nchini kote za kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Taarifa zinasema kuwa wawakilishi hao wa jamii ya Qur'ani watamsomea pia alfatiha hayati Imamu Khomeini na kuweka shada la maua kwenye ziara la mwanzilishi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Jumuiya ya Darul Qur'ani ya Iran imewataka makurai, mahafidhi, walimu na wanaharakati katika masuala ya Qur'ani nchini kuhudhuria kwa wingi shughuli hiyo itakayofanyika katika ziara la Imam Khomeini Mwenyezi Mungu amrehemu. 352692

captcha