IQNA

Kuanza mashindano ya Quran kwa vijana Bangladesh

15:31 - January 27, 2009
Habari ID: 1736575
Mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu maalumu kwa vijana nchini Bangladesh yalinza Jumatatu ya jana katika mji mkuu wa nchi hiyo Dhaka.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kuwait (KUNA), mashindano hayo yameratibiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhisha Qur'ani kwa ushirikiano wa Taasisi ya Kuhifadhi ya Bangladesh.
Mashindano hayo yanafanyika katika viwango vinne yaani, kuhifadhi Qur'ani nzima, kuhifadhi juzuu 20, kuhifadhi juzuu 10 na kuhifadhi juzuu tano.
Vijana 270 wa Bangladesh wanashiriki katika mashindano hayo yatakayoendelea kwa muda wa siku tano.
Kamati ya majaji katika mashindano hayo itajumuisha maimamu na mahatibu wa misikiti ya kitaifa ya Dhaka, Mkurugenzi wa Mahafidh wa Qur'ani wa Bangladesha na Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Kiislamu nchini humo pamoja na wasomaji kadhaa wa Qur'ani nchini humo.
Akizungumza katika sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo, Muhammad Bin Azmullah al Haqib, Mwakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Qur'ani amesema kuwa: “Lengo la kufanyika mashindano hayo ni kuwahimiza vijana na mabarobaro kushikamana zaidi na mafunzo ya Qur'ani na maadili ya Kiislamu. 354468
captcha