Msimamizi wa Idara ya Masomo na Mashindano ya Taasisi ya Wakfu na Masuala ya Kheri ya Iran amesema kuwa mashindano ya kitaifa ya kufafanua maana ya Qur'ani Tukufu yatafanyika katika mikoa yote nchini humo tarehe 5 Februari sambamba na sherere za kuadhimisha miaka 30 ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.