Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Saudi Arabi SPA, sherehe za uzinduzi wa ukurasa huo zilizofanyika Ijumaa zilidhudhuriwa na maafisa wa masuala ya utamaduni wa Saudia.
Akizungumza katika sherehe hizo Abdul Azizi Abdullah Hunfi Mkuu wa Kituo cha Kuhifadhi Qur'ani cha Jumuiya ya Misaada ya Jeddah amesema kuwa: “Katika awamu ya kwanza ya kuanzishwa ukurasa huo, kutakuwa na vitabu 1600 vyenye maudhui ya Qur'ani na makala za utafiti.
Ameongeza kuwa, ukurasa huo wa Intaneti umezinduliwa kwa himaya ya Taasisi ya Utafiti wa Qur'ani ya Al Shatby inayofungamana na Kituo cha Kuhifadhi Qur'ani cha Jumuiya ya Misaada Jeddah.
Abdul Azizi Abdullah Hunfi amemaliza kwa kusema kuwa, watafiti na wasomi wa Qur'ani nchini Saudi Arabia wanaweza kuwasilisha makala zao katika ukurasa huo wa intaneti. 356793