IQNA

Qur'ani ya pili kwa kuwa na umbo dogo zaidi duniani inahifadhiwa nchini Yemen

10:06 - February 08, 2009
Habari ID: 1741587
Nakala ya Qurani ya pili kwa kuwa na umbo dogo zaidi duniani ambayo ina umri wa miaka 117 inahifadhiwa katika mji wa San'aa huko Yemen.
Nakala hiyo ya Qur'ani ina urefu wa sentimita tatu na kurasa 531.
Gazeti la Yemen la al Thaura limeandika kuwa nakala hiyo ya Qur'ani ilichapishwa mwaka 1892 katika taasisi ya uchapishaji ya al Amiriyya nchini Msri na kusimamiwa na Maulamaa wa al Azhar.
Kurasa za Qurani hiyo ndogo zimepambwa kwa sanaa za Kiislamu na imeandikwa kwa hati za Othman Twaha. Katika sehemu ya maelezo kumeandishwa maneno yafuatayo: Nakala hii ya Qur'ani imetolewa zawadi na Hamoud Nasif Bek, Mtawala wa Yemen katika mwaka 1920 Miladia kwa Yahya Aal Hamiduddin, faqihi, mwanahistoria, mhakiki na mwandishi ambaye pia ni miongoni mwa viongozi wa Kialawi wa nchi hiyo.
Qur'ani hiyo iliandikwa na Sheikh Muhammad bin Ali bin Khalaf al Hussaini, Shekhe wa makari wa zama hizo wa Misri na imepitiwa na wasimamizi wa Wizara ya Maarifa ya Misri. Ukurasa wa maelezo wa nakala hiyo ya Qur'ani umetiwa saini ya Sheikh wa wakati huo wa chuo cha al Azhar.
Nakala ndogo kuliko zote ya Qur'ani Tukufu ina urefu wa sentimita mbili na inahifadhiwa nchini Jordan. Nakala hiyo ina umri wa miaka mia moja. Nakala ya tatu kwa udogo ya Qur'ani duniani yenye umri wa miaka 60 iko nchini Indonesia. 360621
captcha