Gazeti la Telegraph limeandika kuwa lengo la kuzalisha wanasesere hao ni kuwafunza watoto wa wahajiri wa Kiislamu nchini Uingereza istilahi za Qur'ani kupitia michezo na kwa njia za kuburudisha.
Mkuu wa shirika linalozalisha wanasesere hao Farzan Rahman amesema: "Nilipokuwa mtoto mdogo nilikuwa nikienda msikitini kila siku kwa ajili ya kujifunza na kuhifadhi Qur'ani, suala ambalo halikuwa na mvuto mkubwa kwangu. Uzalishaji wa wanasesere hawa utawawezesha watoto kujifunza Qur'ani kwa njia za kuburudisha na kuvutia."
Wanasesere hao wanazungumza na kusoma istilahi, ibara na sura za Qur'ani na tarjuma yake ya lugha ya Kiingereza kwa kubonyezwa miguu. 361127