IQNA

Mtalii wa Sweden awaomba radhi Waislamu kwa kuivunjia heshima Qur'ani

13:28 - February 11, 2009
Habari ID: 1742918
Mtalii mmoja wa Sweden katika eneo la Kashmir ambaye alibandika aya za Qur'ani Tukufu juu ya relitheluji zinzotumiwa katika mchezo wa ski, amewaomba radhi Waislamu.
Kituo cha kupasha habari cha PTI kimeripoti kuwa Hans Patric amekutana na mwanazuoni wa ngazi za juu wa eneo la kitalii la Gulmarg huko Kashmir Sheikh Bashiruddin na kusisitiza kuwa kitendo chake kilitokana na uchache wa maarifa na kwamba hakuwa na nia ya kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu.
Awali mtalii huyo wa Sweden aliiambia polisi ya eneo la Kashmir kwamba alibandika karatasi iliyokuwa na aya za Qur'ani aliyopewa na mkewe Muislamu raia wa Qarat kwenye relitheluji hizo bila ya kutambua hatima ya jambo hilo.
Wananchi wa eneo la kitalii la Gulmarg huko Kashim Jumamosi iliyopita walifunga maduka na ofisi zao wakiitaka mamlaka ya eneo hilo kumchukulia hatua mtalii huyo na kulinda heshima ya Qur'ani Tukufu.
Hata hivyo baada ya kutambua kwamba kitendo hicho hakikufanyika kwa nia mbaya na kufuatia hatua ya Patric ya kuomba radhi, Sheikh Bashiruddin amewataka watu wa eneo hilo kumsamehe mtalii huyo. 362264
captcha