IQNA

Kuzinduliwa tovuti mpya ya Jumuiya ya Qur'ani ya Mfalme Fahd nchini Saudi Arabia

15:20 - February 11, 2009
Habari ID: 1743054
Tovuti mpya ya Jumuiya ya Qur'ani ya Mfalme Fahd imezinduliwa katika mji mtakatifu wa Madina kwa lengo la kuwasilisha Qur'ani Tukufu kwa miandiko mbalimbali ya Kompyuta.
Shirika la Habari la Kimataifa la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu IINA limemnukuu Muhammad Salim bin Shadid al-Aufi, Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo akisema kuwa, tovuti hiyo itawasilisha maandishi ya Kiarabu ya Qur'ani kwa wasomaji wake katika miandiko tofauti na kuwapa fursa wasomaji wa tovuti hiyo kuweza kuwasilisha makala zao za kiutafiti kwa njia ya kompyuta.
Al-Aufi amesema kwamba, jumuiya hiyo pia imetayarisha CD maalumu zinazohusiana na masuala ya Qur'ani kwa ajili ya kuwawezesha watu kuweka Qur'ani katika simu zao za mkononi na pia kwenye kompyuta. 362229
captcha