IQNA

Wachapishaji wa "Qur'ani Safi" wahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela nchini Afghanistan

17:11 - February 17, 2009
Habari ID: 1745349
Mahakama ya Rufaa ya Afghanistan imewahukumu kifungo cha miaka 20 jela Waafghani wawili kwa kutarjumi Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kiafghani bila ya matini yake ya Kiarabu ambayo wameiita "Qur'ani Safi."
Kituo cha habari cha Akhbarul Alam kimeandika kuwa Mahakama ya Rufaa ya Afghanistan imetoa hukumu hiyo kwa sababu ya upotoshaji uliomo katika tarjumi hiyo ya Qur'ani kwa lugha ya Kiafghani na madai ya utume yaliyotolewa na watarjumi wake.
Waafghani hao wawili waliojulikana kwa majina ya Amad Ghauth Zalmai ambaye ni mwandishi habari, na Sheikh Qari Mushtaq Ahmad, mwaka 2007 walichapisha tarjumi ya Qur'ani kwa lugha ya Kiafghani bila ya kufanya mlinganisho na matini yake ya asili kisha wakaigawa bure miongoni mwa wananchi.
Tarjumi hiyo ya Qur'ani ilikosolewa mno na wanafikra wa Kiislamu wa Afghanistan ambao waliwataja watarjumi hao kuwa ni makafiri na wakataka wahukumiwe kifo. 365175

captcha