Hayo yamesemwa na Mhariri Mkuu wa jarida na utafiti wa masuala ya Qur'ani Hujjatul Islam Walmuslimin Ahmad Barati ambaye amesisitiza kwamba uhusiano kati ya shakhsia aali ya Mtume Muhammad (saw) na kitabu cha Mwenyezi Mungu ni kama uhusiano wa chombo na kinachowekwa kwenye chombo hicho ambavyo vyote viwili vinapaswa kuwa safi kiasi kwamba usafi na unadhifu wa kila mmoja kati yao unasadikisha usafi wa mwenzake.
Hujjatul Islam Barati ameashiria sifa na hali ya kipindi cha kuteremshwa Qur'ani Tukufu na akasema: Sifa makhsusi za Bara Arabu katika zama hizo zilikuwa na taathira katika kueneza Uislamu. Ameashiria sifa ya Waarabu wa wakati huo ya kupendelea maneo ya kuvutia na yenye mizani na vpimo na uwezo wao mkubwa wa kuhifadhi na kushika mambo kichwani.
Amezungumzia falsafa ya thawabu anazopewa mtu kwa kuhifadhi Qur'ani na akasema: Moja ya hekima ya suala hilo ni kuwahamasisha Waislamu kujifunza maneno ya Mwenyezi Mungu na kuyahifadhi, suala ambalo pia linaibakisha Qur'ani hai baina ya Waislamu na kuilinda na upotoshaji. Amesema kuwa suala la kuhifadhi na kukiandika kitabu cha Mwenyezi Mungu lilipewa muhimu mkubwa katika zama za Mtume Muhammad (saw) kwa kadiri kwamba idadi kubwa ya maswahaba ilihifadhi na kuandika aya za kitabu hicho.
Mhariri Mkuu wa jarida la utafiri wa masuala ya Qur'ani linalochapishwa nchini Iran mesisitiza juu ya umuhimu wa shakhsia ya Mtume Muhammad (saw) na akasema: Qur'ani ni ushahidi wa Utume wa Nabii Muhammad (saw) na Mtume mwenyewe ni ithibati ya kwamba kitabu hicho ni maneno ya Mwenyezi Mungu (sw), hususan kwa kutilia maanani kwamba mtukufu huyo alikuwa mashuhuri katika kaumu ya Waarabu wa kabla ya kubaathiwa kwa jina la 'Muhammad Muaminifu' (Muhammad al Amiin). Kwa msingi huo wakati maneno ya Mwenyezi Mungu yanayosemwa na mtu wa aina hiyo huwa na taathira kubwa zaidi katika nyoyo za watu. 367441