Tangu zamani matabibu wa Kiislamu walikuwa wakitumia aya za Qur'ani Tukufu kutibu wagonjwa, na maandiko ya kidini ya Waislamu yamezungumzia taathira za kitiba za kusoma sura za Fatiha na Tauhidi.
Kwa kuzingatia nyaraka hizo za kidini zenye itibari na imani kubwa ya Waislamu kwa aya za kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu, wataalamu wamefanya uchunguzi na utafiti kuhusu taathira za aya za suratul Fatiha na suratu Tauhidi kwa wagonjwa wa ugonjwa wa Multiple Sclerosis (MS) au ugonjwa wa kukacha kwa seli.
Utafiti huo ulifanywa kwa wagonjwa 12 kwa tabibu kusoma aya za sura hizo mbili na kuweka mikono yake juu ya kichwa cha mgonjwa na maungo yaliyoathiriwa na ugonjwa wa MS.
Kisomo hicho kimefanyika kwa wiki nane na katika kila wiki tabibu alikuwa akimsomea mgonjwa sura hizo mara moja akiwa karibu yake na mara mbili akiwa mbali.
Utafiti huo umekuwa na matunda ya kuridhisha. 366696