IQNA

Seneta wa Marekani amwalika Wilders kuonyesha filamu inayotusi Qur'ani katika Bunge la nchi hiyo

13:55 - February 25, 2009
Habari ID: 1748561
Seneta mmoja wa Marekani amemwalika mtengenezaji filamu ya Fitna inayokitusi na kukivunjia heshima kitabu kitakatifu cha Qur'ani kuonyesha filamu hiyo katika Bunge la Marekani.
Mwaliko huo wa seneta Jon Kyl umetolewa siku chache tu baada ya serikali ya Uingereza kumzuia mwakilishi huyo wa Bunge la Uholanzi kuingia nchi humo ambako alikusudia konyesha filamu ya Fitna katika Bunge la Uingereza.
Uingereza ilimzuia Geert Wildes kuingia nchi humo baada ya kumtaja kuwa anahatarisha usalama wa kijamii nchin humo kutokana na misimamo yake mikali dhidi ya Uislamu.
Seneta Jon Kyl amedai kwamba sababu ya mwaliko wake kwa Wilders ni kutetea uhuru wa kusema!
Filamu ya Fitna inayokitusi kitabu kitakatifu cha Qur'ani imelaaniwa na Waislamu kote duniani. 368866
captcha