IQNA

Dharau ya Wamarekani kwa Qur'ani yawakasirisha Waafghani

10:56 - March 01, 2009
Habari ID: 1749652
Ijumaa iliyopita, maelfu ya wananchi wa Afghanistan walifanya maandamano makubwa wakilalamikia kitendo cha askari wa Marekani walioko nchini humo dhidi ya kitabu chao kitakatifu, Qur'ani Tukufu.
Kwa mujibu wa tovuti ya al-Muslim, kufuatia maandamano hayo, askari usalama wa serikali ya Afghanistan waliwashambulia waandamanaji katika eneo la Ghazni, kusini magharibi mwa mji mkuu Kabul, na kuwajeruhi watu sita kati yao.
Polisi ya Afghanistan imetangaza kuwa imetuma kundi maalumu la askari katika eneo hilo ili kuchunguza dharau hiyo ya askari vamizi wa Marekani dhidi ya Qur'ani Tukufu.
Wakati huohuo, askari usalama wa nchi hiyo wamekadhibisha madai ya kutokea mapigano kati ya polisi na raia wa nchi hiyo. Ripoti zinasema kuwa, siku ya Alkhamisi usiku, askari wa Marekani washambulia msikiti mmoja wa Afghanistan na kishaa kuuchoma moto pamoja na kurarua Qur'ani zilizokuwemo.
Dharau ya askari wa Marekani kwa Qur'ani si jambo geni kwani mwaka 2005 walifanya kitendo kama hicho cha dharau kwa kitabu hicho kitakatifu huko Guantanamo ambapo Waislamu wa Afghanistan pia walilalamikia vikali jambo hilo. 370170
captcha