IQNA

Maonyesho ya filamu ya Fitna yawakasirisha Waislamu Marekani

10:54 - March 01, 2009
Habari ID: 1749839
Maonyesho ya filamu ya iyayokivunjia heshima kitabu kitukufu cha Qur’ani ya Fitna katika Congresi ya Marekani yamekabiliwa na malalamiko makali ya Waislamu nchini humo.
Waislamu wa Marekani wamekusanyika mbele ya jengo la Congresi ya nchi hiyo kupinga filamu hiyo.
Mwakilishi wa Buge la Uholanzi mwenye misimamo ya kufurutu mipaka na anayeupiga vita Uislamu Geert Wilders Alkhamisi iliyopita alielekea Marekani kwa mwaliko wa Seneta Jon Kyl kwa lengo la kuonyesha filamu ya Fitna inayokitusi na kukivunjia heshima kitabu kitukufu cha Qur’ani, suala ambalo limepingwa vikali na Waislamu wa Marekani.
Mwakilishi Muislamu wa Bunge la Marekani Keith Ellison amepinga kitendo cha kuonyeshwa filamu ya Fitna katika bunge la nchi hiyo na akasema, anaunga mkono uhuru wa kusema lakini filamu ya Fitna haina uhusiano wowote na uhuru wa kusema bali ni madharau na hujuma dhidi ya haki za Waislamu.
Seneta Jon Kyl ametetea msimamo wake wa kumwalika Geert Wilders kuonyesha filamu hiyo katika Bunge la Marekani kuwa eti ni kutetea uhuru wa kusema.
Mbubge Geert Wilders wa Uholanzi amekuwa akishambulia itikadi za Kiislamu hususan kitabu kitakatifu cha Qur’ani ambacho amekifananisha na kitabu cha dikteta wa zamani wa Ujerumani Adolf Hitler. Vilevile ametoa wito wa kupigwa marufuku kitabu hicho. 370282
captcha