Muhammad Hujjatiyan amesema kuwa, kusoma na kuhifadhi Qur'ani, kuhifadhi robo ya Qur'ani katika muhula mmoja wa masomo, darsa za maana ya aya za Qur'ani na mashindano ya maudhui za Qur'ani kwa familia ni baadhi ya masuala yatakayowekwa katika ratiba za Jumuiya ya al-Mustafa. Amesema, kuanzishwa kwa taasisi ya usomaji na uhifadhi wa Qur'ani ni masuala mengine ambayo huenda yakatekelezwa nchini humo iwapo pendekezo la kuanzishwa taasisi hiyo litapitishwa na wahusika.
Akiashiria mipango ya jumuiya hiyo ya kuanzisha mashindano ya kimataifa ya usamoji na uhifadhi wa Qur'ani Tukufu pamoja na hadithi za Mtume Mtukufu (saw), Hujjatiyan amesema kuwa mashindanio hayo ni muhimu sana katika kuwafanya washiriki wavutiwe na kisha kuzingatia mafundisho ya Qur'ani.
Muhammad Hujjatiyan amesema, kulea na kuwafundisha walimu wa Qur'ani ni miongoni mwa mipango mingine ya Jumuiya ya al-Mustafa na kuwa masomo hayo yameanza na idadi ya watu 14, ambapo wanane kati yao ndio waliofanikiwa kupata kiwango kinachohitajika cha alama za kuwawezesha kuwa walimu wa Qur'ani na hivyo kupewa vyeti vya kujishughulisha na shughuli hiyo muhimu. Amesema, kuanzishwa vipindi vifupi vya masomo ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu na hadithi ni shughuli nyingine ambayo imekuwa ikifanywa na kitengo hicho. 370547