Hayo yamesemwa na Aliredha Muhammadi mtafiti wa elimu ya Qur'ani na kuongeza kuwa, msimu wa machipuo ni fursa nzuri kwa watu kupate fursa za kukutana na kujumuika na familia pamoja na jamaa zao huku wakiwa wanasherehekea kuwadia kwa mwaka mpya. Amesema kuwa kutembeleana na kuimarishwa uhusiano kati ya familia na jamaa ni jambo lililo na umuhimu mkubwa kadiri kwamba Mwenyezi Mungu ameweka umuhimu wa jambo hilo pembeni ya ibada ya kuabudiwa Kwake kwa ikhalsi kwa kusema: 'Mwabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni ihsani wazazi wawili na jamaa..'
Nasaha nyingi ambazo zimetolewa na Qurani Tukufu pamoja na hadithi za watukufu wa dini kuhusiana na udharura wa kuimarishwa uhusiano wa familia na jamaa ni jambo linalothibitisha wazi umuhimu wake.
Fiqhi ya Kiislamu inasisitiza sana umuhimu wa kuwepo uhusiano mzuri kati ya jamaa wa familia na kusema kuwa jambo hilo ni la lazima katika kila hali, yaani hata iwapo baadhi ya jamaa wa familia watakuwa ni makafiri au murtadi. Kwa ibara nyingine ni kuwa, jambo hilo ni muhimu kiasi kwamba, hata kufru na ufuska haufuti haki ya ujamaa kwa mtu yoyote yule.
Ujamaa unasisitizwa hata katika hali kama hiyo kwa sababu huenda uhusiano huo ukamuongoza mtu na kumfanya arejee kwenye njia iliyo sahihi maishani. 379182