Waziri Maftuh Bisyuni amesema katika msikiti wa Nurul Ikhlasi mjini Jakarta kwamba haijuzu kutumia vibaya aya za Qur'ani na thamani za kidini kwa ajili ya kupata mafanikio katika uchaguzi ujao wa Bunge.
Waziri huyo amewataka wagombea kuwavutia wapigaji kura kwa kueleza sera na mipango yao.
Kwa kuzingatia hamu kubwa ya wananchi wa Indonesia kwa masuala ya kidini, wagombea viti vya Bunge wamekuwa wakitumia vibaya maudhui za kidini kuvutia kura za wananchi.
Asilimia tisini ya watu milioni 230 wa Indonesia ni wafuasi wa dini ya Kiislamu. Vilevile Indonesia ndiyo nchi yenye jamii kubwa zaidi ya Waislamu duniani.
Uchaguzi wa Bunge nchini humo umepangwa kufanyika tarehe 9 Aprili mwaka huu. 380754