IQNA

Washiriki katika mashindano ya Qur'ani ya watoto Saudi Arabia waenziwa

15:06 - March 30, 2009
Habari ID: 1759001
Sherehe za kuwatunuku zawadi washiriki katika mashindano ya taifa ya Qur'ani makhsusi kwa watoto wadogo, zimefanyika leo mjini Riyadh Saudi Arabia.
Mashindano hayo yamewashirikisha zaidi ya watoto wadogo mia moja wa kike na kiume wenye umri wa chini ya miaka 15 kutoka makumi ya shule na jumuiya za masuala ya kheri.
Mashindano hayo ambayo yamefanyika kwa ushirikiano wa Baraza la Ushirikiano wa Ghuba ya Uajemi, yamehudhuriwa pia wanaharakati wa masuala ya Qur'ani kutoka nchi za kandokando ya Ghuba ya Uajemi. Washiriki walishindana kuhifadhi na kusoma tajwidi ya juzuu 10, juzuu 5, zujuu mbili, hizbu moja na juzuu Amma. 381309

captcha