Kazi hiyo imefanyika kwa ufadhili wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Ethiopia.
Makumi ya nakala za Qur'ani zilizoandikwa kwa hati za mkono zilipewa utambulisho na alama maalumu katika shughuli iliyodumu kwa kipindi cha mwezi mmoja na nusu.
Mkataba wa kutimiza kazi hiyo ulitiwa saini mwezi Januari mwaka huu kati ya Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Addis Ababa na Mwenyekiti wa Kituo cha Uhakiki cha Chuo Kikuu cha Addis Ababa. 382436