Idara inayohusika na masuala ya utafiti katika Chuo Kikuu cha Imam Swadiq(as) imeanzisha mradi wa kuagiza, kupokea na kusambaza vitabu bora vinavyohusiana na Qur'ani Tukufu, ikiwa ni katika juhudi zake za kuimarisha na kueneza utafiti wa Qur'ani unaokwenda sambamba na jamii ya sasa.
Idara hiyo itakuwa ikijishughulisha na utafiti wa Qur'ani, uandishi wa makala za kielimu na kiutafiti kuhusiana na maudhui za Qur'ani na pia kuzalisha CD kuhusiana na suala hilo.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, waandishi na watafiti ambao vitabu na kazi zao zitaonekana kuwa bora watashirikiana na idara hiyo katika kutarjumiwa na kuchapisha vitabu vyao.
Ili kupata habari zaidi kuhusiana na suala hili, watu walio na hamu ya kushirikiana na idara iliyotajwa wanaweza kuitembelea kwa kutumia anwani ifuatayo: Bozorgrahe Chamran, Pole Mudiriyat, Daneshgahe Imam Swadiq (as), Muawanate Pajuheshi, Idareye Hamkarihaye Elmi va Bainal Milali au kuwasiliana nayo kwa njia ifuatayo: Sanduku la Barua 159-14655, Simu: 88370143 Fax: 88094915 na E-Mail: Quran@isu.ac.ir. 383102