Kwa mujibu wa gazeti la al-Haqiqatu Duwaliyya la Jordan, Qur'ani hiyo ya Marekani ambayo ina kurasa 366 imechapishwa kwa lugha za Kiarabu na Kiingereza.
Katika utangulizi wa Qur'ani hiyo bandia, kuna ibara isemayo: 'Imetolewa kwa ajili ya ulimwengu wa Kiislamu na hasa ulimwengu wa Kiarabu.' Qur'ani hiyo imesambazwa katika shule za nje za Kuwait na gazeti hilo la Jordan linasema kuwa hatua ya mashirika hayo ya Marekani ya kusambaza Qur'ani hiyo potofu ni vita baridi ambavyo vimelenga kuwapotosha wanafunzi wa shule zilizolengwa.
Kuna opotoaji mkubwa ambao umefanywa katika Qur'ani hiyo ya Marekani na hasa kuhusiana na maneno na ibara zake. Kwa mfano, Bismillah imetarjumiwa kwa maana ya 'baba' na aya nyingine nyingi kupotoshwa kwa makusudi.
Gazeti hilo la Jordan linasema kuwa lengo la mashirika hayo ya uchapishaji ya Marekani ni kuwafanya Waislamu wakufuru aya za Mwenyezi Mungu na hivyo kufuata Injili iliyopotoshwa na Wakristo.
Gazeti hilo limeshangazwa na kimya ambacho kimeonyeshwa na serikali, taasisi, mashirika, wakuu na hata vituo vya Qur'ani vya Kuwait kuhusiana na Qur'ni hiyo ya Marekani. Hii ni katika hali ambayo nchi hiyo ilichukua msimamo wa wazi kuhusiana na makosa ya chapa yaliyopatikana hivi karibuni katika uchapishaji wa Qur'ni nchini humo. 384936