Washiriki hao pia wametaka jumuiya hiyo ianzishe shughuli zake za ndani na katika uga wa kimataifa na kupasishwa sheria zake makhsusi.
Wakurugenzi wa vituo vya Qur'ani katika nchi za Ulaya Mashariki wametoa wito wa kutengwa misaada ya kifedha kwa shule, vyuo na vituo vya Kiislamu vinavyoshugulikia masuala ya Qur'ani na kufunza sayansi ya kitabu hicho kitakatifu.
Vilevile wamechunguza suala la kufasiriwa vitabu vya mafunzo ya Qur'ani, kuwekeza katika vitendea kazi vya kutoa mafunzo hayo na kustawisha mawasiliano kwa lengo la kuimarisha mafundisho ya Qur'ani na sayansi ya kitabu hicho.
Kongamano la wakurugenzi wa vituo vya Qur'ani katika eneo la Ulaya Mashariki limesimamiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO na Jumuiya ya Ulimwengu wa Kiislamu.385643