IQNA

Qur'ani na taaluma zake kufunzwa katika Chuo cha Teolojia cha Kanisa Katoliki Zambia

14:42 - April 13, 2009
Habari ID: 1764331
Somo la Qur'ani, historia yake na sayansi ya kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu litaanza kufundishwa katika Chuo cha Teolojia cha Kanisa Katoliki nchini Zambia. Somo hilo litatolewa na Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Lusaka Asadi Muwahhid.
Maudhui nyingine zitakazofundishwa katika chuo hicho cha Kanisa Katoliki ni Utambuzi wa Mwenyezi Mungu, umoja wa Muumba wa dunia, uadilifu wake, utume, siku ya Kiyama, historia ya Mtume Muhammad (saw), nafasi ya swala na taathira zake katika jamii, saumu na falsafa yake, hija na hekima zake, zaka na jihadi, falsafa ya vazi la hijabu katika Uislamu, sababu ya kuharamishwa kamari na haki za mwanamke katika Uislamu.
Wanafunzi na uongozi wa Chuo cha Teolojia cha Kanisa Katoliki cha Zambia umekaribisha suala hilo.
Mafunzo ya dini ya Kiislamu na dini nyinginezo muhimu duniani ni moja ya masomo yanayotolewa na mapadri kwa wanafunzi wa Chuo cha Teolojia cha Kanisa Katoliki nchini Zambia. Kutolewa mafunzo hayo na mkuu wa kitengo cha utamaduni cha Iran nchini humo kumechangia mno katika kufafanua vyema Uislamu kwa wanafunzi wa chuo hicho. 387003
captcha