IQNA

Qur'ani iliyoandikwa na Imam Kadhim, moja ya turathi zenye thamani kubwa za Kiislamu

13:55 - April 14, 2009
Habari ID: 1764843
Qur'ani Tukufu inayonasibishwa kwa Imam Mussa al Kadim (as) ambaye ni mmoja wa Maimamu Watukufu kutoka Nyumba ya Mtume Muhammad (saw) ni nakala yenye thamani kubwa katika ulimwengu wa Kiislamu na dhihirisho la sanaa ya Kiislamu na Iran.
Sehemu hiyo ya Qur'ani ambayo imepokelewa kwamba iliandikwa kwa hati za mkono wa Imam Kadhim (as) inakusanya aya za kuanzia 252 za suratul Baqarah hadi aya ya 89 ya suratu Al Imran.
Nakala hiyo ina kurasa 83 na kila ukurasa una mistari 6 na maelezo yaliyoandikwa kandokando na ukurasa.
Kurasa za nakala hiyo ya aya za Qur'ani zimetengenezwa kwa ngozi ya swala.
Maandishi ya nakala hiyo ya aya za Qur'ani yameandikwa kwa hati za Kikufi za karne ya tatu Hijria na maneno yake yametengwanishwa kwa kiwango maalumu.
Nakala hiyo ya maandishi ya Qur'ani yaliyoandikwa na mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) Imam Kadhim (as) inahifadhiwa katika jumba la makumbusho la Haram ya Imam Ridhaa (as) mjini Mash'had nchini Iran.387460

captcha