IQNA

Vigezo vikuu vya marekebisho ya mwenendo wa matumizi viko katika aya za Qur'ani

14:49 - April 14, 2009
Habari ID: 1764883
Suala la kuweka wazi vigezo vya marekebisho ya matumizi ya mwanadamu ni jambo la dharura ambalo limefafanuliwa kwa njia bora zaidi katika aya za Qur'ani Tukufu.
Hayo yamesemwa na Hujjatul Islam Hussein Ali Akbarniya, Mkuu wa Idara ya Ulinganiaji wa Kiislamu wa mji wa Shazand nchini Iran. Sheikh Akbarniya amesema kuwa mafundisho ya dini ya Kiislamu yanakidhi mahitaji yote ya mwanadamu na Qur'ani Tukufu na viongozi wa dini wamebainisha mambo mengi katika uwanja huo.
Amesema kuwa, kuna udharura wa kufafanuliwa vigezo vya mwenendo wa kubana matumizi na kufanya iktisadi na kwamba suala hilo linapaswa kupewa umuhimu mkubwa hususan katika mwaka huu ambao Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran Ayatullah Ali Khamenei ameupa jina la mwaka wa Marekebisho ya Mwenendo wa Matumizi.
Hujjatul Islam Akbarniya amesema kuwa ni wajibu kwetu kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto za kiutamaduni na kidini zinazowakabili wananchi. Amesisitiza kuwa kuna udharura wa kuchukuliwa hatua za kuondoa matatizo ya kijamii na kubuni njia za kuyatatua. 387338
captcha