IQNA

Qur'ani iliyoandikwa kwa mkono wa Imam Hassan (sa) katika mji wa Mash'had

22:52 - April 16, 2009
Habari ID: 1765741
Nakala pekee ya Qur'ani inayonasibishwa kwa Imam Hassan bin Ali bin Abi Twalib inahifadhiwa katika jumba la makumbusho ya Qur'ani la haram ya Imam Ridha (as) katika mji mtakatifu wa Mash'had kaskazini mwa Iran.
Nakala hiyo ya Qur'ani ni moja na maandiko yenye thamani kubwa yanayohifadhiwa katika jumba hilo la makumbusho. Qur'ani hiyo imeandikwa kwenye ngozi ya swala na ina juzuu mbili.
Kila ukurasa mmoja wa nakala hiyo ya Qur'ani inayoyasibishwa kwa mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) Imam Hassan (as) ina mistari saba.
Katika ukurasa wa mwisho wa nakala hiyo inayokusanya baadhi ya sura za Qur'ani kuna maneno yanayosomeka: Imendikwa na Hassan bin Ali bin Abi Twalib katika mwaka wa …. 388924

captcha