Naibu Waziri wa Masuala ya Kiislamu wa Maldives Ahmadullah Jamiil amesema kuwa Jumuiya ya Fiqhi ya Kiislamu iliyoundwa hivi karibuni nchini humo itataanza shughuli zake kwa kuunda kamati ya kuchunguza makosa ya tarjumi za Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Dhivehi. Amesema kuwa marekebisho makubwa ya tarjumi hizo ni kuhusu maneno ya lugha ya Kiarabu yaliyotumika katika tarjumi hizo.
Jamiil amesema kuwa hadi sasa Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Maldives imekusanya nakala elfu tu tatu za Qur'ani kwa ajili ya kusahihishwa.
Hii ni katika hali ambayo mwezi Oktoba mwaka jana ofisi ya Rais wa Maldives iligawa nakala laki moja na nusu kwa familia za nchi hiyo. 389958