Sherehe za uzinduzi wa kipindi hicho zimehudhuriwa na maulamaa wa Kisunni na Kishia. Kipindi hicho kinakusudia kutoa muongozo kuhusu njia ambazo Waislamu wanapaswa kutumia ili kufikia na kudumisha umoja.
Ofisi ya Uhusiano wa Umma katika Kanali ya Qur’an imesema kipindi hicho kimetayarishwa na Masoud Khusruzadeh, kwa ushirikiano na Azizullah Ismaili na Jamshid Kalantari.
Kipindi cha “ Njia ya Mola Mmoja” kitakuwa na sehemu 52 zenye dakika 45 kila kimoja na kitajumuisha mazungumzo na mahojiano. Kitarushwa hewani siku za Jumamosi kuanzia saa 12:53.
Lengo la utengenezaji kipindi hicho ni kuandaa mazingira ya kufikiwa umoja miongoni mwa wafuasi wa madhehebu ya Kiislamu, kuleta ukuruba baina ya madhehebu, na kuchunguza njia za kukabiliana na changamoto za umoja wa Kiislamu.
Kipindi hicho kitawajumuisha na kuwaleta pamoja maulamaa waandamizi wa Kisuni na Kishia ambao watajadili umuhimu na udharura wa umoja pamoja na mbinu za kuondoa vizingiti vya kuufikia umoja wa Kiislamu. 393792