Ayatullah Muhammad Ali Muvahidi Kermani Khatibu wa sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesifu na kuwashukuru wananchi wa Iran ya Kiislamu kwa kushiriki kwa wingi katika hamasa ya kisiasa na kueleza kuwa hamasa hiyo ilikuwa itikio kwa wito wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa ajili ya kushiriki katika uchaguzi huo wa rais. Ayatullah Muvahidi Kermani amesisitiza kuwa hamasa ya kisiasa ya Juni 14 2013 kwa mara nyingine tena imelipa heshima na fakhari taifa la Iran na kupelekea kushindwa maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Khatibu wa sala ya Ijumaa ya Tehran pia amempongeza Sheikh Dakta Hassan Ruhani Rais mteule wa Iran na kumtaja kuwa kiongozi shupavu, mfuasi wa utawala wa faqihi na mwenye rekodi nzuri kabla na baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
1245882