Kwa mujibu wa Abdullah Abdulmalik mkurugenzi mkuu wa banki hiyo, hatua hiyo ni katika fremu ya mkakati wake wa kupanua wigo wa shughuli zake katika eneo zima la Kati na Mashariki mwa Afrika ambapo baada ya Tanzania wanatazamia kufungua matawi Uganda na Somalia.
Gulf African Bank inayotoa huduma zake zote kwa mujibu wa sheria za Kiislamu imesema ina wateja 58,000 katika matawi yake yote 14 nchini Kenya. Bw. Abdulmalik amesema wameweza kufikia asilimia saba tu ya Waislamu ambao wanaweza kutumia huduma za banki za Kiislamu na kwa hivyo bado kuna fursa ya kupanua zaidi mfumo wa banki za Kiislamu nchini Kenya na eneo. Mbali na Gulf African Bank, banki ya pili ya Kiislamu nchini Kenya ni First Community Bank
Tayari nchini Tanzania kuna banki mbili za Kiislamu huku Somalia ikitangaza kuwa itahakikisha kuwa mfumo wake wa banki utazingatia misingi ya Kiislamu.
Wakati huo huo Banki Kuu ya Uganda imesema imeandaa pendekezo la kubuniwa sheria za kuruhusu mfumo wa banki za Kiislamu nchini humo. Naibu mkuu wa masuala ya kibiashara katika Banki Kuu ya Uganda Godfrey Yiga Masajja amesema tayari pendekezo hilo litafikishwa mbele ya baraza la mawaziri ili kuidhinishwa.
1249982