Akihutubu katika dhifa hiyo ya futari iliyohudhuriwa na mamia ya Waislamu wa matabaka mbali mbali Jumamosi usiku, Kenyatta alisema hatua yake ya kuwaalika Waislamu kufuturu Ikulu ni njia ya kuonyesha kufungamana kwake na Waislamu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Aidha Rais Kenyatta ametoa mchango wa shilingi milioni mbili kuwasaidia Waislamu wasiojiweza kununua bidhaa wanazohitajia katika mwezi huu mtukufu. Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Rais William Ruto ametoa wito kwa Waislamu kuombea amani Kenya katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Amesema dhifa hiyo ya futari ni fursa kubwa kwa Waislamu kuja pamoja pasina kujali tafauti zao za kisiasa.
Viongozi wa Kiislamu waliozungumza katika hafla hiyo wamemshukuru Rais Kenyatta kwa mwaliko wake na kusema futari katika Ikulu ya Rais ni tukio la kihistoria na ni ishara ya umoja wa kitaifa.
Mawaziri Waislamu Kenya kama vile Najib Balala, Amina Mohammed, Adan Abdallah Mohammed na Dr. Hassan Wario walihudhuria futari hiyo.
1261229