Ayatullah Muhammad Ali Movahhedi Kermani amesema Marekani, utawala ghasibu wa Israel na waitifaki wao wamekuwa wakipiga ngoma za vita dhidi ya Syria lakini wamegundua hatari inayowakabili na ndio maana kwa sasa wameamua kutia ulimi puani. Ayatullah Kermani amesisitiza kuwa, nchi yoyote itakayoanzisha mashambulizi dhidi ya Syria iwe tayari kuungua kwenye moto wa vita hivyo. Ametahadharisha kuwa, Marekani ikijaribu kuingilia kijeshi mgogoro wa Syria itapatwa na aibu kama iliyoupata muungano wa Usovieti miaka ya huko nyuma. Khatibu wa Muda wa Sala ya Ijuma hapa Tehran ameukumbusha Umma wa Kiislamu kwamba, Utawala haramu wa Israel ndio chanzo cha matatizo katika eneo la Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika na kuwataka Waislamu wajiepushe na utawala huo wa Kizayuni.
Huku hayo yakijiri, Balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa, Bashar Ja'afari amesema kuwa, Rais wa nchi yake, Bashar Assad ametoa agizo la kusainiwa mkataba wa WCW unaopinga usambazaji na utumiaji wa silaha za sumu. Itachukua muda kabla ya nchi hiyo kuwa mwanachama ingawa weledi wa mambo wanasema hiyo ni hatua moja mbele kwa Syria kuangamiza silaha za kemikali na kwamba nchi zingine zinapaswa kufuata mkondo huo.
1287190