Duru za usalama za harakati ya Hamas zimesema kuwa, shambulio hilo lililenga kituo cha mafunzo ya kijeshi cha kaskazini mwa Gaza lakini hakuna hasara iliyoripotiwa. Hayo yamejiri baada ya maroketi mawili kuvurumishwa huko kaskazini mwa mji wa Ashkelon, ulioko kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Katika upande mwingine, Wizara ya Afya katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa maisha ya maelfu ya wagonjwa yako hatarini, kutokana na ukosefu wa dawa unaosababishwa na mzingiro wa Israel. Wizara hiyo imesema wagonjwa 400 wanaosumbuliwa na matatizo ya kutofanya kazi figo wamekosa dawa na kemikali maalumu zinazohitajika kwa ajili ya kusafishwa damu.
Utawala wa Kizayuni wa Israel tangu mwaka 2007 unazingira Ukanda wa Gaza, suala linalowapelekea wakaazi wa Kipalestina wa eneo hilo kuishi kwa mateso makubwa. 1309067