IQNA

Ewe Mwenyezi Mungu, Kwa hakika nakuomba umsalie Muhammad SAW. Mtume wa Rehma zako na neno la nuru yako, Ujaze moyo wangu nuru ya yakini, na kifua changu nuru ya Imani.
Ewe Mwenyezi Mungu, Kwa hakika nakuomba umsalie Muhammad SAW.
Mtume wa Rehma zako na neno la nuru yako, 
Ujaze moyo wangu nuru ya yakini, na kifua changu nuru ya Imani.
Zijaze fikra zangu nuru ya nia,
Ijaze irada yangu nuru ya ujuzi,
Ijaze nguvu yangu nuru ya vitendo,
Na ujaze ulimi wangu nuru ya kusema kweli,
Ijaze dini yangu nuru ya ufahamu wako,
Ujaze uono wangu nuru. 
Yajaze masikio yangu nuru ya hekima,
Yajaze mahaba yangu nuru ya kumpenda Mtume Muhammad SAW na watu wa nyumba yake.
Mafatihul Jinan, Ziara ya Aal Yaseen

Ziara ya Aal Yaseen