IQNA

Misri yatangaza sheria ya kutotoka nje wiki mbili kukabiliana na corona

23:14 - March 24, 2020
Habari ID: 3472598
TEHRAN (IQNA) – Misri imetangaza sheria ya kutotoka nje kuanzia saa moja usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi kuanzia Jumatano kwa muda wa wiki mbili ili kukabiliana na kuenea kwa kasi uongjwa hatai wa COVID-19 maarufu kama corona.

Katika taarifa, Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Mabouly amesema atakayekiuka sheria hiyo ataadhbiwa vikali kwa mujibu wa sheria za hali ya hatari nchini humo.

Aidha shelu pamoja na vyuo vikuu vitaendelea kufungwa kwa muda wa wiki zingine mbili na hivyo kuongeza muda wa ile amri ya awali ya kufungwa wiki mbili kuanzia Machi 14.

Aghalabu ya huduma za uma na idara za serikali zitaendelea kufungwa katika kipindi chote cha kutekelezwa sheria ya kutotoka nje na idadi ya wafanyakazi wa serikali wanaoripiti kazini pia itaendelea kupunguzwa hadi kati kati ya mwezi Aprili.

Serikali ya Misri imetengea wizara ya afya dola milioni 63 kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 ambao hadi sasa umeua watu 19 nchini humo huku wengine 366 wakiambukizwa.

3470980

captcha