Kwa mujibu wa tovuti ya Al-Mesriyoon, Osama al-Hadidi, Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Fatwa cha Al Azhar, amesema wanaougua Corona wanaharamishwa kuhudhuria katiak Sala ya Ijamaa ili kuzuia mgonjwa kuwaambukiza waumini ugonjwa huo hatari.
Kuhusu uwezekano wa kupigwa marufuku kwa muda sala ya ijumaa au sala za jamaa misikitini nchini Misri, amesema uamuzi utachukuliwa baada ya ushauri kutoka kwa wataalamu.
Aidha amesema Al Azhar itaisaidai wizara ya afya Misri katika kuudhibiti ugonjwa wa Corona.
Idadi ya walioambukizwa Corona hadi sasa nchini Misri imefika 55.