IQNA

Futari misikitini marufuku Misri katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

9:00 - April 05, 2020
Habari ID: 3472635
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Wakfu nchin Misri imetangaza kuwa ni marufuku kuandaa futari kwa umma misikitini katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Katika taarifa, Wizara ya Wakfu Misri imetoa wito kwa wahisani ambao wamekuwa wakiwapa waumini futari misikitini miaka iliyopita kutumia fedha hizo kuwasaidia wasojiweza na wanaohitajia misaada katika jamii.

Wizara ya Wakuf ya Misri imeashiria sunna nzuri  ya jamaa kujuliana hali katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kutoa wito kwa watu kuwasaidia majirani au jamaa wasio na uwezo.

Katika tahadhari hiyo ambayo imetolewa zikiwa zimesalia takribani siku 20 kabla ya kuanza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Wizara ya Wakfu y Misri imesema imetoa tangazo hilo mapema ili wahisani wasianze kujitayarisha kwa ajili ya dhifa za futari misikitini.

Hadi kufikia sasa zaidi ya watu 1,000 wameambukizwa corona nchini Misri huku wengine 71 wakiwa tayari wameshafariki dunia.

3889121

captcha